KIKONGWE AOMBA BIA AKIWA KARANTINI | Tarimo Blog

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
OLIVE Veronisi (93) mkazi wa Pittsburgh Pennsylvania ameteka mitandao ya kijamii baada ya picha yake akiwa na kopo la bia na bango lenye ujumbe wa "Nahitaji bia zaidi" kusambaa na kupendwa na  watu wengi zaidi.

Mwanamke  alionekana kutokea dirisha la nyumba yake akitekeleza agizo la kutotoka nje (lockdown) ikiwa ni sehemu ya kupambana na virusi vya Corona (Covid -19) vilivyosambaa kote duniani.

Imeelezwa kuwa picha hiyo ambayo ilichukuliwa na jamaa zake imetazamwa zaidi ya mara milioni 4 katika mtandao wa Facebook jambo lililopelekea kampuni ya vinywaji ya Morson coors kumpa alichokuwa anahitaji.

Mapema jumatatu Olive alipokea kopo150 za bia kutoka Molson Coors ambapo msemaji wa Molson Coors Darren Rovell amesema kuwa baada ya kuona ujumbe huo waliamua kuungana na mtu aliyeleta tabasamu usoni mwa watu wakati wa janga hili la Corona na wamemshukuru Olive kwa kuwa shabiki wa kinywaji cha Coors Light.

Mara baada ya kupokea zawadi hiyo Olive alikuja kivingine kwa kushika bango lililosomeka "Nimepata bia zaidi."

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2