
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imetoa msaada vitu mbalimbali katika Taasisi ya Ocean Road vyenye thamani ya zaidi ya sh.milioni Tano (5).
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa katika kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo watoe msaada kwa kutambua Ocean Road ili kuweza kuwasaidia wagonjwa waliopo hapo.
Profesa Mgaya amesema kuwa licha ya kutoa msaada huo wataendelea kuwa karibu zaidi katika utoaji wa misaada mbalimbali.
"Tunaadhimisha Maadhimisho haya lakini tumetambua Ocean Road umhimu wa kuchangia nguvu zetu katika kuwasaidia wagonjwa kwani wanatoka sehemu mbalimbali ya nchi yetu na wakati mwingine wanaweza wakawa na changamoto ambazo sio za kimatibabu"amesema Profesa Mgaya
Profesa Mgaya amesema katika Maadhimisho hayo wamefanya shughuli mbalimbali ikiwemo upimaji afya kwa wananchi bure kwa magonjwa ya kuambukiza na yale yasioambukiza.
Baadhi ya vitu walivyokabidhi ni sabuni za kuogea,Sabuni za Kufulia,Sabuni za Unga,Dawa za Meno,Maji,Maziwa ya Kopo ,Taulo,Kanga,Magauni aina ya Madela pamoja vifaa tiba.
Nae Kaimu Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Beatrice Erasto amesema Kama Taasisi wanatoa shukrani kwa NIMR kutoa msaada kwao.
Amesema kuwa wanachangamoto lakini wadau wanapowaunga mkono katika kuwasaidia wanawatoa sehemu moja kwenda nyingine.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment