BODI YA MIKOPO KUFUNGUA DIRISHA LA KUKATA RUFAA (APPEAL) KWA WAOMBAJI WA MIKOPO MWAKA 2016/2017

Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu Tanzania (HESLB), imewatangazia waombaji wote wa mikopo kwamba itafungua dirisha la kukata rufaa (APPEAL) kwa siku 90 kuanzia tarehe 31 oktoba 2016.
Waombaji wote watatakiwa kufuata hatua zifuatazo:
  1. Waombaji wote watatakiwa kulipia shilingi 10,000/= ambayo haitarudishwa, kwa kila rufaa kupitia Mpesa kabla ya kukata rufaa
  2. Waombaji watatakiwa kujaza fomu ya kukata rufaa ambayo ipo mtandaoni, na kuambatanisha na nyaraka zote muhimu zinazohitajika. Fomu za rufaa zinapatikana kwenye hii link hapa http://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/olas/login
  3. Baada ya kujaza fomu ya rufaa, waombaji watatakiwa kuituma fomu hiyo pamoja na nyaraka zote muhimu katika dawati la ofisa wa bodi ya mikopo katika Taasisi zao.
  4. Rufaa zote zitatakiwa kupitia kwa ofisa wa mikopo katika taasisi husika ambao watazikusanya fomu hizo na kuziwasilisha bodi ya mikopo. Bodi ya mikopo haitakubaliana na rufaa ambazo zitakusanywa na mwanafunzi binafsi.
  5. Mwisho wa kukusanya rufaa ni tarehe 31 Januari 2017.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na tangazo hili, bofya hapa kwenye link hapa chini kuliona tangazo hili
http://www.heslb.go.tz/index.php/application-guidelines/226-appeals-against-means-test-results-for-2016-2017

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2