MPYA KUTOKA TCU

SERIKALI IMETANGAZA SECOND ROUND APPLICATION KWA KIDATO CHA SITA, STASHAHADA NA RPL 2016/2017
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

 
Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja waudahili tarehe
31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba
udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
 Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali
mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe
12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.

  • Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
  • Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
  • Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
  • Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 namatokeo yao yameshatoka,
  • Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
  • Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.
Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu taratibu zingine za
kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2