NCHI NA MIPAKA VIPO SALAMA, TUTAMLINDA RAIS SAMIA - CDF MABEYO | Tarimo Blog

 


Na Leandra Gabriel, Dar es Salaam

MKUU wa Majeshi Tanzania CDF Venance Mabeyo amesema hadi sasa  nchi na mipaka yake  ni salama na wataendelea kumlinda  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CDF Mabeyo ameyasema hayo leo Machi 26 wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Joseph Magufuli Wilayani Chato mkoani Geita ambapo amesema kuwa kwa niaba ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini anahakikisha uimara wa ulinzi na usalama ambao pia utaendelea kuimarishwa.

"Tutaendelea kukulinda ukiwa Rais wa Tanzania na Amiri jeshi mkuu na sio Amirati kama ilivyokuwa inapendekezwa, vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kukutii na kutekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.'' Amesema CDF Mabeyo.

Aidha Mabeyo amesema vyombo vya ulinzi vinamhakikishia Rais Samia  uadilifu, utii na uaminifu kwa mujibu wa mila na desturi za majeshi katika kuhakikisha ulinzi na usalama kama ilivyokuwa katika awamu zote za uongozi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2