Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu imetangaza ya kwamba, kwa sasa imemaliza zoezi za kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017ambalo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016. Pia imetangaza kwanba inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.Pia iinawakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.
http://www.heslb.go.tz/index.php/application-guidelines/222-taarifa-kwa-waombaji-wa-mikopo-kuhusu-kumalizika-kwa-zoezi-la-kurekebisha-taarifa-za-waombaji
Post a Comment