KUTOKA BODI YA MIKOPO-TAARIFA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017

Leo mapema, bodi ya mikopo ya Elimu ya juu Tanzania (HESLB) imetangaza kwamba imekamilisha zoezi la la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016.Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika
mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknolojia.
bodi imetangaza kwamba, vigezo hivyo ni pamoja na
1. Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya  Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni:-
       • Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
       • Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
       • Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
       • Sayansi Asilia, na
       • Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.

2. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima.
3.Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha.
Bodi ya mikopo imeorodhesha majina ya waombaji wenye uhitaji, waliopata mikopo, ambayo ni pamoja na;     
  • Wadahiliwa yatima waliopata mkopo                                                       873
  • Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo                                                   118
  • Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja                                           3,448
  • Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali                     87
  • Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele                         6,159
  • Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine                                      9,867
  • Jumla                                                                                                   20,183
KIASI CHA FEDHA ZINAZOHITAJIKA
Katika taarifa iliyotangazwa na bodi ya mikopo,Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hali kadhalika, bodi ya mikopo imetangaza hatua zinazofuata ikiwa ni pamoja na;
  • Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo.
  • Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao. 
  • Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
Tangazo hili limetolewa na
                       MKURUGENZI MTENDAJI
                                     BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tembelea hii link hapa chini kulipata tangazo hili na kwa uhakika zaidi
http://www.heslb.go.tz/index.php/application-guidelines/225-utoaji-wa-mikopo-kwa-wanafunzi-mwaka-2016-2017
 

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2