Tume ya taifa ya vyuo vikuu nchini imetangaza awamu ya nne ya
kufanya maombi ya kujiunga na Elimu ya juu nchini.Tume imetangaza kwamba, baada
ya kukamilisha mchakato wa maombi ya waombaji wa vyuo vikuu, vyuo Vikuu
Vishiriki na Taasisi za elimu ya juu kwa awamu ya Kwanza, ya Pili na yaTatu,na
matokeo ya waombaji wote waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni kukamilika,imebaini
kuwa bado kuna waombajakribani 5,301 ambao bado wako kwenye mfumo na
hawajakamilisha maombi yao.
Pia tume imetangaza kwamba, imebaini kuwepo kwa idadi kubwa
ya waombaji hasa wenye Stashahada ambao hawakuomba kabisa kutokana na matokeo
yao ya mitihani kuchelewa kufika Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE).
awamu hii itawahusu: Waombaji ambao bado wako ndani ya mfumo
ambao hawajachaguliwa, Waombaji wapya ambao hawakuwahi kuomba awali pamoja na
waombaji walio na sifa linganifu,ambao hawakukamilisha taratibu za uombaji hapo
awali.
Tume imetangaza kwamba, Kutokana na sababu tajwa hapo juu,
itafungua Mfumo (CAS) kwa siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi
Jumatano tarehe 26 Oktoba 2016 ili kuruhusu Makundi tajwa hapo juu kuingia
kwenye mfumo.
Pia Tume imewataka waombaji wa awamu ya nne kuzingatia,
Kuhakikisha wanaomba kozi walizo na sifa stahiki, Kuhakikisha wanakamilisha
maombi yao kiufasaha, na kuhakikisha wanajiridhisha na nafasi zilizopo kwa
kuzingatia viwango valivyofaulu.
Pia, tume imetangaza kwamba a Umma kwamba kozi zote
zisizoonekana kwenye mfumo kwa sasa kuwa zimejaa.Baada ya tarehe tajwa hapo juu
Tume itafunga rasmi zoezi la udahili kwa mwaka 2016/17 ili kuruhusu mchakato
mingine ya Bodi ya Mikopo na Vyuo.
Tangazo hili limetolewa
Kaimu katibu mtendaji,
Tume ya vyuo vikuu Tanzania
21/10/2016
Hii hapa link kupata undani wa tangazo hili zaidi
Post a Comment