BARAZA LA TAIFA LA UFUNDI (NACTE) LAVIFUNGIA VYUO 26 VYA UFUNDI

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26 kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE, Dkt.Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo.
“Kama ilivyoelezwa katika sheria za Usajili na Kanuni za leseni, kutozingatia matakwa yoyoye yaliyowekwa na NACTE ni kosa kisheria.
 Kanuni zinasema kuwa hatua kali zinawezakuchukuliwa kwa kila kosa. Kulingana na matokeo ya ufuatiliaji uliofanywa na timu maalumu, Baraza lina uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya taasisi au vyuo vinavyoshindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa,” alisema.

Alisema kuwa baada ya kufanya utafiti wao, wamebaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,
wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.
“Baraza linaufahamisha umma kwamba limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo vya ufundi 48 kutokana na makosa mbalimbali, yaliyofanywa na vyuo hivyo ambapo limesitisha vyeti vilivyotolewa kwa vyuo 20 ambavyo vimeshindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye Cheti cha Usajili.
“Uamuzi huu umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 20 ya Usajili wa Vyuo vya Ufundi ya mwaka 2001,” alisema.
Rutayuga alisema kwamba vyuo vilivyofutiwa usajili kutokana na kosa la kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika ni 26.
“Vyuo vya ufundi vinatakiwa kupata kwa idhini ya Baraza kabla ya kuanza kutoa mafunzo yoyote. Idhini hiyo inahusu uthibitisho wa mtaala kwa ajili mafunzo yaliyokusudiwa na utambuzi wa idara iliyopangwa kutoa mafunzo hayo,” alisema.
Juu ya vyuo vyenye vituo vya setelite, kampasi, Dkt.Adolf Rutayuga alisema kuwa Baraza linahitaji mafunzo kutolewa katika vituo vilivyosajiliwa/kampasi za vyuo vikuu baada ya kuthibitishwa kwamba vinastahili kutoa mafunzo.
“Hata hivyo, taasisi mbili zimebainika kutoa mafunzo katika vituo vya satellite/vyuo vikuu ambavyo havijasajiliwa na Baraza na hivyo kuadhibiwa. Vyuo hivyo navyo vimefutiwa leseni,” alisema Rutayuga.
Orodha 1: Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili
S/N CHUO
1 Institute of Management and Development Studies – Iringa
2 Green Hill Institute – Mbeya
3 Institute of Business and Social Studies – Mbeya
4 Loyal College of Africa – Mbeya
5 Mbeya Training College – Mbeya
6 Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga
7 New Focus College – Mbeya
8 Shukrani International College of Business and Administration – Mbeya
9 Majority Teachers College – Mbeya
10 Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga
11 MAM Institute of Education – Mbeya
12 Belvedere Business and Technology College – Mwanza
13 Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita
14 Global Community College – Geita
15 Muleba Academy Institute – Muleba
16 St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita
17 Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza
18 Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza
19 Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam
20 SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam
21 Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara
22 Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha
23 Emmanuel Community College – Kibaha
24 Modern Commercial Institute – Dar es Salaam
25 Marian College of Law – Dar es Salaam
  Orodha 2: Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa
S/N CHUO MAFUNZO
1 MISO Teachers College – Mafinga Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
2 Tusaale Teachers College – Mafinga Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
3 The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro
4 The Golden Training Institute – Dar es Salaam
5 Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma
6 National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha
7 Musoma Utalii Training College – Musoma
8 Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza
9 Mwanza Polytechnic Institute – Maswa
10 Ruter Institute of Financial Management – Mwanza
11 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza
12 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita
13 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba
14 Singni International Training Institute – Bukoba
15 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama
16 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu
17 Richrise Teachers College – Geita
18 Twiga Training Institute – Musoma
19 Zoom Polytechnic Institute – Bukoba
20 St. Thomas Training College – Shinyanga
  Orodha 3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi
S/N CHUO
1 MISO Teachers College – Mafinga
2 Rungemba Teachers College – Mafinga

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2