Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa sababu
mbalimbali ikiwamo kutowasilisha ripoti za ukaguzi wa hesabu za fedha.
Sababu nyingine ni kutokuwa na ofisi na kushindwa kuthibitisha kuwa na wanachama ZanzibarAmevitaja vyama hivyo ni Chama cha Haki na Ustawi (CHAUSTA) kilichokuwa kinaongozwa na James Mapalala na The Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) kilichokuwa kinaongozwa na Peter Mziray kama Rais Mtendaji.
Chama kingine kilichofutiwa usajili ni Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari kama Mwenyekiti taifa
Source: Mwananchi
Post a Comment