Tarehe 12/12/2016 wizara ya elimu, sayansi na teknolojia ilitangaza kuwa wahitimu wa stashahada na shahada za ualimu katika masomo ya sayansi (fizikia, kemia, biolojia) na hisabati wa mwaka 2015 wawasilishe vyeti vyao kwa ajili ya uchambuzi wa wahitimu wenye sifa.
Wahitimu waliokuwa na mapungufu katika nyaraka zao wanatakiwa wawasilishe tena. Wahitimu hao ni kama ifuatavyo:-
1. Waliotuma nakala za “results slips” au “academic transcripts” bila nakala za vyeti halisi vya kidato cha 4, 6, stashahada au shahada
2. waliotuma nakala za vyeti vya stashahada za uzamili (postgraduate diploma in education – pgde) bila nakala za “vyeti vya shahada ya kwanza pamoja na “academic transcripts” zake;
3. Wahitimu ambao hawakutuma kabisa nakala za vyeti vyao wanapewa fursa ya mwisho kutuma.
Bonyeza hapa kupata majina ya wahitimu wa shahada na stashahada waliowasilisha vyeti
ORODHA YA WAHITIMU WA SHAHADA
ORODHA YA WAHITIMU WA STASHAHADA
Wahitimu waliopo
kwenye orodha hapo juu wasiwasilishe nyaraka hizo tena.
Utaratibu wa
kutuma vyeti ni kama ifuatavyo:-
1.
Waombaji lazima
‘wa-scan’ vyeti halisi (original certificates - kidato cha 4, 6, stashahada,
stashahada ya uzamili au shahada) na siyo kivuli cha cheti (photocopy) ;
2.
Waombaji wa
stashahada ya uzamili (pgde) na shahada lazima ‘wa-scan’ na kutuma nakala za
“academic transcripts” za shahada ya kwanza.
3.
Waombaji lazima
waweke nakala za vyeti vyao vyote kwenye ‘file’ moja likiwa katika ‘pdf’ na
lipewe jina la mwombaji husika kabla ya kutuma. Nyaraka zitumwe kupitia ‘barua
pepe’ zao wenyewe na siyo za watu wengine.
Tanbihi:
Waombaji watume taarifa zao kupitia barua pepe ya
wizara info@moe.go.tz
Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 17 januari,2017.
Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji
zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu wa kutafuta
zilizo sahihi.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
PROF. SIMON S. MSANJILA
KAIMU KATIBU MKUU
TANGAZO KWA WAHITIMU WA STASHAHADA NA SHAHADA
Post a Comment