kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa
kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa
Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni
mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China.
amesema kuwa kongamano hilo linatarajia kufanyika Oktoba 25,2017 katika hoteli
kubwa yenye hadhi ya nyota tano jijini Beijing,litakalojumuisha wafanyashabiashara
wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao
200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda, na kwa njia moja ama
nyingine iweze kuzigeuza rasimali maliasili kuwa bidhaa”alisema Kilua.
mazao ya Chakula na Biashara,haiwezi kutafsiri maendeleo hayo ya Kilimo bila
kuzigeuza bidhaa zilizoandaliwa kwa soko la ndani na lile la Kimataifa bila
kuwepo na viwanda vidogo/vya kati na vikubwa vitakavyozalisha bidhaa zenye
viwango vyenye ubora katika ushindani wa soko”alisisitiza Kilua.
Viongozi hao ni Mkurugenzi wa halmashauri Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani (kofia nyekundu), Mansouly Ally ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha, Afisa Biashara (M) Pwani Suleiman Sirindwa, Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Mhina.
Viongozi hao wamekuja jijini Beijing nchini China kwa ziara iliyoratibiwa na Kampuni ya Kiluwa Group of Companies,chini ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wake Mohamed Said Kiluwa (mwenye koti la njano) kwa ajilia kushiriki Kongamano kubwa la Viwanda.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhina akikata kipande cha nyama ya Mbuzi,ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha wageni na wenyeji kwenye chakula cha jioni kiliochoandaliwa na wenyeji wa Beijing,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua,kulia ni Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja na Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga wakishuhudia tukio hilo usiku huu.
Baadhi ya wenyeji ambao nao wanatarajiwa kushiriki kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika Octoba 25,2017 chini ya Uratibu mkubwa wa kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies,jijini Beijing nchini China.
Wageni wakipewa maelezo mafupi katika baadhi ya michoro ambayo walipewa kama zawadi kutoka kwa wenyeji wao,kabla ya kupata chakula cha jioni pamoja.
SOMA ZAIDI
Post a Comment