Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Pwani wakipatiwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huateng Metalluargical Co.Ltd, Chunsheng Jiang (wa tatu kulia) kuhusiana na michoro waliyopewa kama zawadi, ikionyesha mandhari ya maeneo mbalimbali ya jiji la Beijinga pamoja na shughuli zao nchini China. Viongozi hao ni Mkurugenzi wa halmashauri Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani (kofia nyekundu), Mansouly Ally ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha, Afisa Biashara (M) Pwani Suleiman Sirindwa, Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga (koti jekundu) pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Mhina. Viongozi hao wamekuja jijini Beijing nchini China kwa ziara iliyoratibiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa (mwenye koti la njano). Malengo ya ziara hiyo ni kuja kuangalia fursa za viwanda zilizopo Beijing kwa kushirikiana na wadau wakubwa waliopo mjini humo na hatimaye fursa hizo kuzileta nyumbani nchini Tanzania kuendeleza na kuunga mkono juhudi za rais za kujenga uchumi wa viwanda
Aidha baada ya kukutana leo viongozi hao pamoja na wadau wakuu wa mambo ya viwanda nchini China, kesho wanatarajia kushiriki kwa pamoja mkutano utakaohusu masula ya viwanda,utakaojumuisha wadau zaidi ya 160 kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.
from Michuzi Blog
Soma Zaidi
Post a Comment