Helikopta iliyoanguka Ziwa Nakuru mara baada ya kuruka kutoka katika hoteli jirani na ziwa hilo Jumamosi hii asubuhi imepatikana lakini habari zinasema miili ya abiria watano waliokuwamo bado haijapatikana.
Habari zinazidi kueleza kwamba helikopta hiyo ilikuwa ikielekea kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha Jubilee katika county ya Narok.
Ajali hiyo ilithibitishwa na kitengo cha Taifa cha maafa cha Kenya (NDMU). "Taarifa toka chanzo cha kuaminika ni kwamba kwa bahati mbaya helikopta binafsi imezama katika ziwa Nakuru, na inadhaniwa kwamba abiria na nahodha wake bado wangali wamenasa ndani yake.
"Juhudi za uokoaji zinaendelea na NDMU imeleta helikopta kusaidia zoezi hilo", Naibu Mkurugenzi wa NDMU Mwachi Pius amenukuliwa akisema.
Polisi bado haijatoa majina ya watu watano walikuwemo kwenye ajali hiyo hadi baada ya ndugu wao wa karibu kujulishwa.
from Michuzi Blog
Soma Zaidi
Post a Comment