YANGA YAWASHA MOTO SHINYANGA ‘AJIB AMKIMBIZA KIMYAKIMYA OKWI’

22549658_503126883400428_9177873523110656274_n

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Mzunguko wa Saba imeendelea Leo kwa Mchezo mmoja kupigwa kwenye dimba la Kambarage mkoani Shinyanga kwa wenyeji Stand United kukubali kichapo cha magoli 4-0 toka kwa Mabingwa Watetezi Yanga.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 24 kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Ibrahim Ajib Migombo aliyepiga faulo ya moja kwa moja na kumuacha kipa wa Stand, Frank Muwonge  hana la kufanya Obrey Chirwa alitoa pasi ya bao kwa Ajib dakika ya 30 na kuwafanya mashabiki wa Yanga walipuke kwa shangwe.

Baada ya kuingia kwa magoli hayo mawili Stand walianza kujilinda na kuwapa mwanya Yanga kutawala Mpira katika eneo la kati lililokuwa chini ya Pato Ngonyani na Papy Tshishimbi ambao walionekana kuelewana vyema hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa magoli mawili.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo Yanga walifaidika na mabadiliko hayo katika dakika ya 54 Yanga walipata bao la tatu likifungwa na kiungo mshambuliaji Pius Buswita akifunga kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na winga wa pembeni Geoffrey Mwashiuya.

Wakiendelea kutuma salama kwa mahasimu wao Simba,Mshambuliaji mwenye kasi uwanjani Obrey Chirwa alipigilia msumari wa nne kwa kazi nzuri iliyofanywa na Ajib na kutoa pasi ya bao kwa Mzambia huyo likiwa bao la mbili kwake hadi mwamuzi Erick Onoka kutoka Arusha aliyesaidiwa na Omary Juma na Vincent Mlabu,akimaliza Mpira Yanga wameibuka na ushindi wa magoli 4-0.

Aidha huu ni ushindi mkubwa kwa Yanga tangu Ligi ianze kwani walikuwa hawajapata ushindi mnono kama huo na kwa matokeo hayo wamefikisha jumla ya pointi 15 na kushika nafasi ya pili na Simba wakiwa bado wanaongoza Ligi kwa kuwa na pointi kama hizo wakiwa na wastani mzuri wa magoli ya kufunga,Mtibwa  wakiwa na 15 nafasi ya tatu.

Tazama Msimamo wa Ligi Kuu baada ya Michezo ya Mzunguko wa saba:

22728979_503206770059106_177607837493152942_n


SOMA ZAIDI

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2