BALOZI SOKOINE AKUTANA NA WATANZANIA UBELGIJI

Zamototz
Balozi wa Tanzania nchi Ubelgiji Mh:Edward Joseph Sokoine katikati akiwa na baadhi ya watanzania waliofika jana kwenye kikao cha kusikiliza na kutafutia ufumbuzi kero za watanzania wanaoishi nje ya  Tanzania. {Picha zote na Maganga One Blog} 
Kiongozi wa Watanzani kitongoji cha Antwerpen nchini Ubelgiji ndugu Joseph Makani akimkaribisha Mh Balozi na maafisa Ubalozi alioambatana nao hapa jana,kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi ndugu Shoo na upande wa kulia ni afisa ubalozi ndugu Juma Salum.Kikao kilikwenda vizuri kwani kila mmoja alipewa fursa ya kuuliza maswali. {picha zote na Maganga One Blog} 
Afisa Ubalozi ndugu Juma Salum{kulia}akitoa ufafanuzi wa swali aliloulizwa kuhusu maswala ya hati za kusafiria pindi mtu anapotaka kurudi nyumbani,alielezea kwa kirefu taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili mtu kuepuka usumbufu. 
Mh Balozi akimsikiliza mmoja wa watanzania ndugu Omari Songambele {hayupo pichani}aliyetaka ufafanuzi kuhusu Uraia Pacha. 
Baadhi ya kina mama wa Kitanzania na nchi jirani walihudhuria mkutano uliowakutanisha na Balozi Sokoine 


from Michuzi Blog
Soma Zaidi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2