DC MLOZI: MADIWANI FUATILIENI MAKUSANYO KATIKA STENDI YA TABORA KUZIBA UPOTEVU

NA TIGANYA VINCENT

RS TABORA

MADIWANI na Watumishi wa wa Manispaa ya Tabora wameagizwa kufuatilia makusanyo ya katika  Stendi za Mabasi ya Tabora ili kujua mapato halisi yanayopatikana kila siku kwa ajili  kudhibiti upotevu wa makusanyo katika stendi hiyo na kuiongezea Halmashauri hiyo makusanyo yake ya ndani.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi wakati akizungumza na Madiwani na Watumishi wakati wa kikao maalum cha kujadili rasmi ya mpango wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Alisema kuwa ni vema watembelea Stendi hiyo na kuangalia utaratibu unatumika katika ukusanyaji mapato kutokana na magari yanapita na yale stendi hiyo ili kujua fedha taslimu zinapatikana na kwa mwaka jambo litakalowawezesha kujua Halmashauri inatakiwa ipate kiasi gani.

“Waheshimiwa Madiwani nawaombeni sana muangalie upya makusanyo katika vyanzo vyenu mbalimbali kama vile stendi na matangazo ili kujiridhisha kama Halmashauri inachopata kinalingana na hali halisi au kuna mianya ya upotevu ili tuizibe mapema” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alisema kuwa hatua itawasaidia kutekeleza maelekezo ya viongozi ikiwemo yale ya Waziri Mkuu ya kutaka kila Halmashauri kuhakikisha inakusanya sio chini ya 80 ya mapato yake ya ndani kila mwaka nje ya hapo viongozi watawajibishwa.

Queen aliongeza kuwa haipendezi kwa Halmashauri kama Tabora kujieleza kwa kushindwa kufikia lengo wakati inaweza kubuni vyanzo mbalimbali ambavyo vitawasaidia kuvuka lengo.

Alisema kuwa wanaweza kuanzisha eneo maaalumu kwa ajili ya  wafanyabiashara (Machinga) kila mara moja kwa wiki ambalo linaweza kuwa chanzo kingine cha mapato.

Naye Diwani wa Kata ya Ng’ambo George Mpepo aliwaomba Madiwani wenzake kuufanyia kazi ushauri wa Mkuu huyo wa Wilaya kwa sababu utawasaidia kuongeza makusanyo na kuwa na fedha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wakazi wa Manisapaa ya Tabora.

Alisema kuwa haipendezi kuona Halmashauri nyingine zinavuka lengo huko kila mwaka inashindwa na kuongeza kuwa wakiendelea kushindwa ni vema Baraza hilo la Madiwani livunjwe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ushauri wako umenigusa sana…naomba wenzangu tukayazingatie hayo…na kama tutashindwa nitakuomba umuombe Waziri Mkuu avunje Baraza hilo la Madiwani kwa kushindwa kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo kuifanya Manispaa ya Tabora iendelee kuwa nyuma” alisema Mpepo.


SOMA ZAIDI

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2