Zamototz
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongea na Mahabusu wa Gereza Keko(awapo pichani) leo Januari 28, 2018 alipotembelea gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini.
Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah akitoa taarifa fupi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa kabla ya kumkaribisha kuongea na Mahabusu wa Gereza Keko(hawapo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimsikiliza Mahabusu ambaye ni raia wa kigeni mara baada ya kuongea na Mahabusu wa Gereza Keko.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akikagua jiko la gesi katika Gereza la Mahabusu Keko. Jeshi la Magereza tayari limeanza kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuachana na matumizi ya kuni kwa kutumia nishati ya gesi katika baadhi ya magereza nchini hivyo kutunza mazingira.
from Michuzi Blog
Soma Zaidi
Post a Comment