
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeeo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Nyasaka Manispaa ya Ilemela baada ya kuwakabidhi baadhi hati miliki za radhi baada ya makazi yao kurasimishwa.
……………………………………………………………….
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameziagiza taasisi zote za serikali kuhakikisha mwaka huu zinayapima maeneo yake ili kuepusha migogoro ya ardhi baina yao na wananchi.
Alisema maeneo hayo yakisha kupimwa yawekewe vigingi na pillars za kudumu kuepuka yasivamiwe tena huku akiwataka waliojenga ndani ya eneo la uwanja wa ndege wa Mwanza kuondoka na waelezwe wazi kuwa ni wavamizi.
Lukuvi alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na watumishi wa idara za Ardhi za Mipango Miji za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
“Tumechoshwa na migogoro ya wananchi na serikali inayohusu ardhi na hivyo kila taasisi ya umma, iwe Hifadhi , mashamba ya mifugo, magereza Jeshi la Wananchi na polisi yapimwe ili serikali ijue wanamiliki maeneo gani maana wengine wanayatumia kuzalisha lakini hawatulipi kodi kwa kuwa hayajapimwa,”alisema Lukuvi.
Alieleza kuwa mwaka huu anataka kuondosha migogoro ya wananchi na serikali na kufafanua kuwa taasisi nyngi za umma haziyatabui maeneo zinayoyamiliki na ndio maana anataka yapimwe na kuondokana na migogoro na wananchi ili kila mmoja asimamie eneo lake.
Aidha,waziri huyo alizuia kubomolewa kwa nyumba za wananchi wa eneo la Kigoto katika Manispaa ya Ilemela lenye mgogoro kati yao na polisi na wala wasibughudhiwe kabla ya uamuzi kutolewa na serikali.
“Nilikuja kwa ajili ya migogogoro mikubwa ule wa Kigoto wa kutaka kuwaondoa wananchi na kuna mapendekezo.Kwa macho yangu nimeona polisi wanaweza kuishi wote na wananchi,”alieleza waziri huyo na kuongeza:
“Tunaweza kuwaondoa ama kuwabakiza na polisi nao wapate eneo la ujenzi wa nyumba zao wanazozitaka kwa hivyo nitakwenda kujadiliana na viongozi wangu na ninasitisha zoezi la kuwaondoa na wasisumbuliwe na kusiwe na ujenzi mpya hadi uamuzi mwingine wa serikali utakapotolewa.”
Pia viwanja vilivyokuwa vimepimwa katika eneo la Nyashana linalomikiwa na JWTZ viwanja hivyo vifutwe na kama kulikuwa na waliokuwa na title deal na kama wapo waliokuwa wamepewa hati tutashirikiana na kuwapa viwanja vingine.
Lukuvi pia aliwataka wakulima wa mboga mboga ndani ya hifadhi ya uwanja wa ndege waondoke ndani ya wiki moja kuanzia sasa wakati serikali ikiaangalia jinsi ya kufanya baada ya kubaini nyumba za watu waliovamia eneo hilo na kujenga nyumba za makazi na jinsi ya kuwafanya.
SOMA ZAIDI
Post a Comment