Wajumbe wa Bunge la Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya walipotembelea TBL ARUSHA

Wajumbe wa Bunge la Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya, mwishoni mwa wiki walifanya ziara ya kutembelea kiwanda cha bia cha TBL cha Arusha ambapo walishuhudia shughuli za uzalishaji zinazoendeshwa na mifumo ya kisasa na teknolojia za hali ya juu .
 
Akiongea  na ujumbe huo,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Arusha,Joseph Mwaikasu, alieleza  jinsi kampuni ya TBL Group mbali na kufanya uzalishaji kwa kutumia  mifumo na teknolojia za kisasa katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Arusha,Mbeya na Dar es Salaam inatekeleza sera  ya ‘Dunia Maridhawa’ (Better world) ambayo imelenga kukuza viwanda  sambamba na kuboresha shughuli za utunzaji wa mazingira , vyanzo vya maji na kuboresha maisha ya watu kwenye jamii ambapo kampuni imewekeza.
“Sera ya Dunia Maridhawa malengo yake yanashabihiana na Malengo Endelevu ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (SDG’s) na sisi kama kampuni tunahakikisha tunafanikisha  malengo haya na kwa kiasi kikubwa tumepata mafanikio hususani katika maeneo ya kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira,matumizi mazuri ya maji ,kuendesha kampeni za utunzaji wa vyanzo vya maji,matumizi ya nishati mbadala zisizo na athari kwa mazingira,kuharibu taka kwa kutumia teknolojia za kisasa, na utakatishaji wa maji taka”.Alisisitiza Mwaikasu.

TOUR TBL ARUSHA 1

Wajumbe hao wakitembelea eneo la Kiwanda

TOUR TBL ARUSHA 5

Meneja wa kiwanda cha TBL cha Arusha,Joseph Mwaikasu,akiwaelezea  mfumo wa uendeshaji kazi wa viwanda vya TBL Group

TOUR TBL ARUSHA 7

Picha mbalimbali zikionyesha wajumbe wakipata maelezo ya mchakato wa utengenezaji bia kutoka kwa wataalamu wa vitengo mbalimbali

TOUR TBL ARUSHA 8 TOUR TBL ARUSHA 9 TOUR TBL ARUSHA 10 TOUR TBL ARUSHA 11 TOUR TBL ARUSHA 12


SOMA ZAIDI

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2