WARIDI LA MAPENZI
SEHEMU YA TATU
Ilipoishia
SEHEMU YA TATU
Ilipoishia
Kwa mbali waliweza kumuona Suma akija huku amebeba mikoba
yake. Alipofika kitu cha kwanza alimuuliza Mwalimu GG kama amemuona Sosi kwani
alikuwa anamtafuta na hawezi kuondoka. Akaambiwa Sospeter ameshafika hapo na
yuko ndani ya basi.
Endelea..........................
Penzi
lao lilikua taratibu na miaka miwili baadaye walifunga pingu za maisha kabla tu
ya kuanza masomo ya Chuo Kikuu. Waliishi pamoja Dar-es-Saalam wakati wote wa
masomo hadi walipohitimu shahada zao za kwanza mwaka 1998. Wote waliajiriwa
jijini hapo, Sospeter akifanya kazi katika idara ya Takwimu huku Suma akipata
nafasi ya Ualimu katika shule ya sekondari ya Lugalo. Watu walionea wivu kwa
jinsi walivyokuwa chanda na pete wakipendana kuliko kumbikumbi au njiwa.
Waliheshimiana na kusaidiana katika kila hali. Ndio uchungu huu uliokuwa
umekita kwenye moyo wa Suma akiwa bado amelala kitandani. Machozi yaliendelea
kumbubujika.
“Suma,
Suma, amka” Sauti ya upole ya kiume ilimshtua usingizini.
“Mume wangu Sosi” Suma aliendelea kulia huku akigalagala kitandani.
“Nini tena Suma, mbona unalia usingizini” Sauti hiyo iliendelea kuuliza huku mikono ya mtu huyo ikimtikisa, “umeota jinamizi mpenzi” Iliendelea sauti hiyo.
“Mume wangu Sosi” Suma aliendelea kulia huku akigalagala kitandani.
“Nini tena Suma, mbona unalia usingizini” Sauti hiyo iliendelea kuuliza huku mikono ya mtu huyo ikimtikisa, “umeota jinamizi mpenzi” Iliendelea sauti hiyo.
Suma
hakuamini kusikia sauti hiyo, kwani haikuwa sauti ya mtu mwingine isipokuwa ya
mume wake wa ndoa Sospeter Mkiru. Alifumbua macho yake taratibu kuangalia kama
alikuwa bado anaota au ni kweli. Sospeter alikuwa ameketi kwenye ukingo wa
kitandani huku akimuangalia mkewe kwa hofu na mahaba makubwa. Hajawahi kumuona
akilia usingizini hata mara moja. Moyoni alijua ndoto yoyote aliyokuwa ameota
hinti huyo ilikuwa ni mbaya kweli.
“Mpenzi,
haya ni ndoto gani hiyo imekufanya ulie usingizini” alihoji huku kwa kutumia
kidole gumba akimfuta machozi Suma.
“Jamani,
hivi ni wewe kweli?” Suma aliinuka taratibu akaanza kuupapasa uso wa Sosi
kuamini kama kweli ni yeye. Kwa mbali aliweza kusikia sauti za watoto zikicheza
mchezo ya kombolela huku mlio wa magari ulisikika kwa mbali ukishindana na
sauti za watoto hao. Alikuwa amelala na kanga moja tu kwani alijitupa kitandani
baada ya kuoga akimsubiri mumewe atoke kazini.
“Ni
mimi mpenzi” Sospeter alijibu kwa upole huku akimrushia busu. Alikumbuka mara
ya kwanza kumbusu Suma miaka ile kule Karatu. Busu lake lilikuwa bado tamu na
lenye mvuto usiochuja. Suma alimkumbatia mumewe na kumwomba Mungu amuepushe na
mikosi yote, na maneno yote ya wamtakiao mabaya. Aliamua kumsimulia ndoto yake.
Alipomaliza, alimuangalia mpenzi wake na kusubiri atasema nini.
“Mama
Grace, tangu nikuone wewe kule Karatu sijaona mwanamke mwingine” Alisema kwa
sauti ya kumhakikishia. “sijatamani wala sijaota kutamani mwanamke mwingine.
Wote ninaowaona nikiwalinganisha na wewe, nitaendelea kukuchagua wewe hadi
kaburini” Alisema huku macho yake yakilengwa na machozi. Suma alijikuta
anatokwa na machozi tena, ingawa safari hii yalikuwa ni ya huba na furaha.
Alimuuliza Mungu ilikuwaje astahili mwanamme namna hiyo.
Suma
aliinuka kitandani, na kabla hajasimama vizuri kanga yake iliyokuwa bado
imemning’inia mwilini ilidondoka, na kumwacha mtupu kama alivyozaliwa. Mwili
wake wenye rangi ya maji ya kunde uliangaza kama mbalamwezi. Sosi alimuangalia
mara moja na hamu yake ikamzidia. Alimvuta karibu huku yeye akiwa bado ameketi,
alifungua miguu yake na kumsimamisha Suma katikati yake huku mikono yake ikiwa
imezunguka makalio ya mviringo wa tufe. Alianza kumbusu tumboni , mapajani,
huku vidole vyake vikiendelea kuyaminya minya makalio ya binti huo. Suma
alinyanyua mguu wake wa kushoto na kuuweka juu ya ukingo wa kitanda. Harufu ya
uanamke wake ilimwingia Sosi kama manukato ya thamani kutoka Yemeni. Kama fundi
wa kukuna, Sosi alianza “kukuna nazi” na kukuna alikuna! Suma aliamua kujitupa
kitandani, na kwa mahaba yasiyokifani walishirikiana tendo la ndoa bila hofu ya
kubambwa au kufaminiwa. Hiyo ndiyo ilikuwa raha ya ndoa. Walipomaliza
walijikuta wamelowa jasho utadhani walikuwa wanakimbia mchakamchaka.
“Haya
niambie safari yako ya hospitali ilikuwaje” Sospeter alipata akili ya kuuliza
kwani Suma alikuwa aonane na Daktari kwa uchunguzi wa kawaida.
“Una
uhakika unataka kujua” Aliuliza kwa sauti ya upole iliyoficha jambo.
“Kido,
nisingeuliza kama nisingetaka kujua” Alisema huku akimgeukia mkewe na kumtazama
usoni. Suma aliuma mdomo wa chini kwa aibu za kike. Alimwangalia mumewe kwa
mapenzi na kwa hamu.
“Unakumbuka
wale mapacha uliokuwa unawazungumzia?” alimuuliza kwa haraka. Ulikuwa mtego
ambao Sosi alinaswa kirahisi.
“Mapacha
gani” aliuliza bila kujumlisha mbili na mbili.
“Kurwa
na doto” Suma alijibu akicheka na kumuangalia usoni. Kama mtu aliyezibuliwa
Sosi alifungua macho yake utadhani yako tayari kuchomoka kama ya Scooby Doo!
“Acha
utani mama Grace!” Alisema
“Wala
sikutanii, nimebeba mapacha!” Alisema kwa fahari kama mtu aliyetimiza wajibu
wake. Sospeter alianza kucheka, kufurahi, na kushangilia utadhani amefunga goli
lililoipeleka timu yake kwenye kombe la dunia Ujerumani! Alimvuta mke wake
karibu na akiweka mkono wake kwenye tumbo la Suma, aliomba sala ya shukurani na
baraka kwa viumbe hao wa Mungu. Mawazoni alianza kutafuta majina kama wote
wakiwa wa kike, wa kiume au mchanganyiko. Suma alienda bafuni pembeni mwa
chumba chao ambako alijisafisha na kubadili nguo. Alipotoka alikuwa anawaka.
Alivalia gauni lake la rangi ya zambarau ya kifalme lenye madoa meupe,
lilikokatwa kifuani kwa mtindo wa V na hivyo kuonesha kontua za matiti yake.
Lilikuwa fupi lililombana kiunoni na kuishia magotini. Nywele zake zilizokuwa zimesukwa
rasta zilidondoka mageni mwake utadhani binti ya mfalme. Alikuwa amejitia rangi
nyekundu ya mdomo na wanja wa kope na nyusi. Alimalizia kwa kutinga viatu vyake
vyenye ndefu kiasi huku vikiwa na kamba zilizozunguka miguu yake. Alikuwa na
usafiri wa nguvu. Alisimama mbele ya kioo huku akijivisha hereni na mkufu
uliokuwa na kito cha Tanzanite kifuani. Sospeter alijikuta akienda na kusimama
nyuma yake, akimkumbatia toka nyuma, Suma alizungusha shingo yake na midomo yao
ikagusana kwa busu lenye utamu wa pepo.
“Grace
amesheenda kwa shangazi yake” Aliuliza Sosi
“Binamu
zake walikuja kumchukua mara tu baada ya kutoka shule” Alijibu Suma. Jioni hiyo
Sosi alimwambia wataenda kwenye ukumbi wa muziki ambako wana Sikinde walikuwa
wanapiga. Suma alitangulia, na kufungua mlango wa mbele. Alipofungua nusura
moyo wake ulipuke kwa mshtuko. Mbele yake kulikuwa na gari jeupe la kifahari la
Limo, huku dereva wake akiwa ameshikilia mwamvuli mbele ya nyumba hiyo, akiwa
naye amevalia suti nadhifu ya rangi nyeupe. Waswahili walikuwa wamekaa nje ya
nyumba zao wakisubiri muda huo. Suma alimgeukia mpenzi wake na kupiga kelele ya
furaha, machozi yakimtiririka tena. Waswahili walijikuta wakipiga makofi na
vigelegele. Sospeter alimnong’oneza mpenzi wake, “Happy Valentine my love”! Suma
aliishiwa nguvu. Waliingia ndani ya gari huku waswahili na watoto wa mtaani
wakipiga minja na vigelegele. Moyoni, Suma aliapa atamrudishia fadhila mumewe
usiku huo.
Mwisho

Post a Comment