Waziri wa Viwanda na Biashara ampongeza mjasiriamali mtanzania aliyebuni kifaa maalumu cha kunawia mikono ili kujikinga na virusi vya Corona | Tarimo Blog

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (Mb) leo tarehe 30 Machi, 2020 amepokea kifaa maalumu cha kunawia mikono kilichotengenezwa na mjasiriamali wa kitanzania ndugu. Jonas Urio (Ambaye anatokea katika mkoa wa Manyara).
 
Akizungumza leo Waziri Bashungwa amempongeza Jonas Urio kwa ubunifu wake huo wa kutengeza kifaa kizuri na bora cha kunawia mikono ambacho kinaweza kutumiwa na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuhudumia watu mbalimbali kusafisha mikono yao ili kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wake Mjasiriamali Jonas Urio ambaye ni mbunifu wa teknolojia hii ameishukuru Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kumpa ushirikiano tangu awali alipoanza ubunifu wake hadi kufikia hatua hii ambapo ameshasajiliwa na ubunifu wake utambulika.
 
Jonas amesema, “Napokea ushauri wa maboresho ya kifaa hiki niliyopewa na Waziri na Naibu waziri ambao wote kwa pamoja wamefurahia sana ubunifu wangu, naahidi kufanyia kazi maboresho yote haraka ili kifaa hiki kingie sokoni ili kusaidia wananchi kujisafisha mikono na kupambana na ugonjwa huu wa Corona”

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2