MKUTANO wa siku tatu uliokuwa unafanyika kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro umemalizika leo Machi 26 mwaka huu wa 2020 kwa mafanikio makubwa.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari imeeleza mkutano huo wa siku tatu ulikuwa ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala na moja ya majadiliano yalikuwa ni kuangalia utaratibu wa Usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugaji na miradi inayotekelezwa katika tarafa za Ngorongoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imefafanua mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo za Wizara ya Maliasili na Utalii na kuongeza majadiliano yamekwenda vizuri na kupata muafaka ambao umefungwa mkono na pande zote na hivyo kusainiwa la kwa mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa yale ambayo wamekubaliana.
Mbali ya Waziri Dk.Kigwangala na maofisa wengine wa Wizara hiyo pia wengine waliokuwepo ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Mfaume Taka, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Profesa Abiud Kaswamila.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Rashid Mfaume Taka, (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Prof. Abiud Kaswamila mara tu baada ya kumaliza mkutano wa kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro .
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment