Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imezindua wimbo maalum wenye lengo la kuhamasisha Wanataaluma kujiunga na Bodi hiyo sambamba na kutoa elimu kwa umma kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Godfred Mbanyi amesema wimbo huo umejikita zaidi Wanataaluma kujisajili na Bodi na kufanya Mitihani ya Bodi na kubobea zaidi katika Taaluma hiyo.
Mbanyi amesema wimbo huo umetoa ujumbe mahsusi wa majukumu, kazi ambayo Bodi imepewa katika kuongeza ufanisi wa majukumu hayo kuongeza tija katika dhima ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda.
“Wimbo huu tutaufanyia uzinduzi katika Matamasha ya Vyuo na Shule mbalimbali katika Makongamano ya Wataalamu baada ya janga hili la Corona kupungua au kuondoka, pale ambapo Serikali itakapotoa ruhusa ya mikusanyiko tutafanya uzinduzi katika Vyuo vinavyotoa taaluma ya Ununuzi na Ugavi”, amesema Mbanyi.
Wimbo huo unapatikana katika Mitandao ya Kijamii ya Bodi hiyo (PSPTB) katika Tovuti (https://www.psptb.go.tz/) na Instagram (psptbofficial), Facebook (Bodi Ununuzi) na YouTube (PSPTB TV).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) , Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua wimbo wa Bodi hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment