Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani DAWASA wamechukua tahadhari kwa wafanyakazi dhidi ya Maambukizi ya homa ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona.
Dawasa wamechukua tahadhari hiyo kwa kuwapatia wafanyakazi wake wakiwemo mafundi wa maeneo mbalimbali vifaa vya kuwakinga ikiwemo Barakoa ili wavae muda wote wakiwa katika majukumu yao.
Hatua hiyo ni muhimu katika kutii agizo la serikali kwa kuvaa barakoa ili kuweza kujikinga, kupunguza maambukizi pamoja na kuwalinda wengine pindi wanapotoa huduma kwa jamii.
Afisa biashara msaidizi DAWASA Noel Kipera akisoma mita ya mteja katika eneo la Kimara stop over huku akiwa amevaa (barakoa), kifaa cha kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona. Dawasa inahakikisha usalama wa watumishi wake dhidi ya maambukizi ya Corona.
Mafundi wa DAWASA Mkoa wa Ubungo wakizibiti uvujaji katika eneo la Mbuzi 40 Kimara kwa kubadilisha mabomba ya nusu inchi. Mafundi hao wametii agizo la serikali kwa kuvaa barakoa kujikinga na maambukizi dhidi ya virusi vya Corona.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment