Mkuu wa wilaya Arusha Fabian Daqarro akipata maelezo ya ujenzi wa Zahanati ya Baraa hali iliyomlazimu kuhoji kusuasua kwa ujenzi wa Zahanati hiyo kama ilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha.
Pichani ni Jengo la Zahanati ya Baraa iliyopo kata ya Baraa jijini Arusha
Msafara ukiwasili kwenye Zahanati ya Baraa
Sehemu ya muonekano wa Jengo lote la Zahanati ya Baraa kama lilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro amehoji kusuasua kwa ujenzi wa zahanati ya Baraa uliosimama kwa zaidi ya miaka 12 wakati halmashauri ya Jiji la Arusha imeshatoaa zaidi ya sh, milioni 84.120 kwa ajili ya ujenzi huo.
Daqqaro alihoji hayo jana Kata ya Baraa wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, Afya na Miradi ya Kimkakati (TSCP) iliyoambatana na wataalam wa Jiji la Arusha.
Alihoji katika kipindi cha miaka 12 wananchi wa kata ya Baraa wamekosa huduma ya Afya na kulazimika kufuata huduma hiyo katika kata zingine kwa kutembea umbali mrefu ."Nataka kujua ni kwanini ujenzi umechukua muda mrefu huku wananchi wakishindwa kupata huduma za afya katika eneo la karibu na makazi yao"
Kaimu Mhandisi wa jiji la Arusha ,Samuel Mshuza alisema awali kulikuwa na vipaumbele vingine vilivyopelekea zahanati hiyo kutokamilika kwa wakati pia ramani ya jengo hilo ilibadilishwa lakini sasa wapo katika hatua za mwisho za ujenzi wa zahanati hiyo
Naye Mtendaji wa Kata hiyo ya Baraa, Anna Lebisa alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ulianza kutekelezwa mwaka 2008na kusimama kwa zaidi ya miaka 12 lakini hivi sasa wanaishukuru serikali kwa kutekeleza ujenzi huo kwa zaidi ya asilimia 86.Huku akisema eneo hilo kunachangamoto ya udongo sambamba na maji kutuama
Hata hivyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk, Maulid Madeni alisema kuwa fedha za ujenzi wa zahanati hiyo zipo na kuwataka wakandarasi wa zahanati hiyo ya Baraa na Hospitali ya Wilaya ya Arusha kusema wanahitaji kiasi gani cha fedha ili waweze kulipwa na ujenzi uendelee
Namshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali na vituo vya afya Mkoa wa Arusha ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru iliyopo Jijini Arusha
Pia Alisisitiza jengo la wadi ya kinamama na mtoto katika hospitali ya wilaya kumalizika mapema ili kuondoa msongamano katika hospitali nyingine
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment