DKT GETRUDE RWAKATARE AZIKWA KANISANI KWAKE MIKOCHENI B | Tarimo Blog

Sanduku lenye mwili wa Askofu na Mbunge wa Viti maalum CCM Mkoa wa Morogoro mama Getrude Rwakatare likiwa tayari kuingizwa kaburini huku likiwa limefunikwa bendera ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar Ea salaam leo.

Baadhi ya Waombolezaji wachache wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Askofu na mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Morogoro Mama Getrude Rwakatare yaliyofanyika kwenye kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar Ea salaam leo.

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro na Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assembly of God (Mlima wa Moto), Mama Getrude Rwakatare leo amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika Kanisa lake lililopo Mikocheni B,Kinondoni jijini Dar.

Waombolezaji waliohudhuria ni wachache wakiwemo wawakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na baadhi ya ndungu kuepuka msongamano kutokana na kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2