GENERAL PETROLEM (GP) YATOA MSAADA WA VYAKULA KUWASAIDIA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI TEMEKE | Tarimo Blog


Katibu Tarafa ya Mbagala Bertha Minga(katikati) ambaye amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lihaniva akipokea msaada wa vyakula mbalimbali kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya General Petroleum (GP) Zafar Khan(kulia) pamoja na ofisa mwingine wa kampuni hiyo.Msaada huo wa vyakula unakwenda kutolewa kwa wananchi wenye kipato cha chini ndani ya Wilaya hiyo.
Bertha Minga ambaye ni Katibu Tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam(kushoto) akiwa na Meneja Mauzo wa Kampuni ya General Petroleum Zafar Khan (kulia) wakati wa makabidhiano wa msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ndani ya Wilaya ya Temeke jijini.
Katibu Tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam Bertha Minga akizungumza baada ya kupokea msaada wa vyakula mbalimbali kutoka Kampuni ya General Petroleum kwa ajili ya kwenda kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini wilayani Mbagala.Minga alikuwa amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lihaniva wakati wa kupokea msaada huo.
Bertha Minga ambaye ni Katibu Tarafa ya Mbagala(kulia) na Ofisa Mtendaji Chamazi Theodor Malata(katikati) wakimsikiliza mmoja wa maofisa wa Kampuni ya General Petroleum baada ya kupokea msaada wa vyakula kutoka kwa kampuni hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ndani ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya General Petroleum (GP) Zafar Khan akiwa ameshika moja ya mfuko wenye chakula wakati anaelezea aina ya vyakula ambavyo kampuni yake imeamua kutoa msaada kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya msaada wa vyakula ambavyo vimetolewa na Kampuni ya General Petroleum kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini vikiwa ndani ya gari kabla ya kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.



Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya General Petroleum ya jijini Dar es Salaam imetoa msaada wa vyakula vya aina mbalimbali vyenye thamani ya Sh.Milioni 50 kwa kuzisaidia kaya zaidi ya zaidi 1,500 za kipato cha chini ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wananchi hao wanapata chakula hicho katika kipindi hiki kigumu ya ugonjwa wa Covid-19.

Kwa mujibu wa Kampuni hiyo ni kwamba inatambua kuwa kutokana na uwepo wa Covid-19 kuna baadhi ya kaya ambazo zinashindwa kufanya kazi zao za kila siku kwa ajili ya kujipatia kipato, hivyo wameona haja ya kutoa msaada huo na hasa kwa kuzingatia Serikali ya Awamu ya Tano moja ya majukumu yake ni kusaidia watu wa kipato cha chini.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lihaniva ambaye aliwakilishwa na Katibu Tarafa ya Mbagala Martha Minga, Meneja Mauzo wa Kampuni ya General Petroleum Zafar Khan amesema wamekuwa na utamaduni wa kusaidia jamii na katika kipindi hiki cha janga la Corona wameamua kuungana na Serikali kwa kutoa msaada huo wa vyakula kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wanyonge.

"Kwa sasa tumetoa msaada wa vyakula kwa kaya 1,500 za jijini Dar es. Salaam na Bagamoyo.na Tumeanza na Wilaya ya Temeke ambapo msaada huo utakwenda kwenye kata zote kutokana na utaratibu ambao umewekwa na Wilaya,"amesema Khan na kufafanua msaada huo unahusisha vyakula mbalimbali pamoja na mafuta ya kupikia.

Kwa upande wake Katibu Tarafa ya Mbagala wilayani Temeke Bertha Minga ametoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo kwani umekuja wakati muafaka na wameonesha kuunga mkono kwa vitendo kusaidia wanyonge kama ambavyo imekuwa kauli mbili ya Rais Dk.John Magufuli ambaye amejikita kusaidia Watanzania wanyonge.

Amesema kampuni hiyo imekuwa na upendo mkubwa kwa wananchi kwani kabla ya kutoa msaada wa vyakula , ilshatoa pia vitakasa mikono na barakoa kwa ajili ya watumishi wa Wilaya ya Temeke pamoja na wananchi mbalimbali kwenye kata zote ndani ya Wilaya hiyo.

Amesema kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke tunaishukuru kampuni hii kwani katika Wilaya yetu wamekuwa na msaada mkubwa sana. Mara zote wamekuwa ni watu wakujitoa kwa ajili yetu,"amesema Minga.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2