JUMUIYA YA MABOHORA TANZANIA WAMKABIDHI RC MAKONDA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA. | Tarimo Blog

Jumuiya ya Dawoodi Bohora Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vya kujikinga na corona vyenye thamani ya Shilingi Milioni 27 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa lengo la kuwakinga wananchi wa Mkoa huo.

Akipokea Vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dr. Rashid Mfaume amesema miongoni mwa vitu vilivyotolewa ni pamoja na Vifaa vya kuzuia maambukizi, vifaa vya kinga binafsi, vyakula vya kujenga mwili, sabuni, dawa za kunawa mikono na mashine za kuua mazalia ya bacteria.

Aidha Dr. Mfaume amesema vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ambapo amewataka wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari na kufuata kanuni na maelekezo yanayotolewa  na Wizara ya Afya.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jumuiya ya Mabohora Bw. Murtaza Adamjee amesema Jumuiya hiyo itaendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Mkoa huo katika mapambano dhidi ya Corona ambapo pia wameipongeza Serikali kwa jitiada wanazozifanya kukabiliana na corona.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2