KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YACHANGIA MSAADA WA LITA 1,250 ZA VITAKASA MIKONO KUUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA, | Tarimo Blog

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengenti, Bw. John Wanyancha sehemu ya lita za Vitakasa mikono,ambapo kampuni hiyo imetoa lita 1,250 ya vitakasa mikono nyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukiza ya virusi.

====== ========== ======== ========

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imeunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa homa ya mapafu maarufu kama Covid-19 kwa kutoa msaada wa lita 1,250 za vitasa mikono. Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu. 

“Tunaamini msaada huu utawasaidia watakaoutumia kuwa salama dhidi ya virusi hatari vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu au Covid-19,” alisema Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa kampuni hiyo John Wanyancha. 

Hii ni mara pili kampuni ya SBL inaiunga mkono Serikali katika Mapambano dhidi ya Covid-19. Wiki mbili zilizopita, SBL ilishirikiana na Wizara ya Afya kusambaza vipeperushi vyenye kutoa elimu ya kujikinga na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu katika sehemu mbali mbali nchini na kuvikabidhi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya mbali mbali. 

Pamoja na mchango huo, Wanyancha alisema kampuni ya SBL inatoa vitakasa mikono na barakoa kwa wafanyakazi wake wa mauzo, kiwandani pamoja na wasambazaji wa bidhaa za kampuni hiyo waliopo sehemu mbali mbali nchini ili kuwawezesha kufanya kazi katika mazingira salama. Kampuni ya SBL inawafanyakazi 800 na mamia ya wasambazaji waliotapakaa kila kona ya nchi. 

Akipokea msaada huo, Waziri Mwalimu aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuiunga mkono Serikali katika vita dhidi ya virusi vya Corona na kusisitiza kuwa vita hiyo inahitaji kuunganisha nguvu ili kuishinda. 

“Vita dhidi ya virusi vya Corona ina changamoto kubwa kwa kila mtu na kila mahali. Vitaa hii pia ina gharama kubwa na kwa hiyo ni lazima tuungane. Tusimame pamoja ili tuweze kuokoa maisha yetu na ya ndugu zetu, “ alisema Waziri Ummy.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2