madiwani Tandahimba wailalamikia tarura kuhusu ubovu wa Barabara vijijini. | Tarimo Blog

Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Tandahimba wameridhia baadhi ya fedha za miradi ya maendeleo kutumika katika shughuli za kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid - 19)

Hatua hiyo wamefikia katika kikao Cha Baraza ambalo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Tandahimba

Aidha madiwani wamesema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Wilaya dhidi ya kuhakikisha wananchi wao pia watachangia fedha ambazo zitasaidia kununulia vifaa mbalimbali  vya kujikinga na uginjea wa Corona

Mbali na Hilo madiwani hao wameomba Wakala wa Barabara vijijini na mijini (Tarura) kutengeneza baadhi ya barabara ambazo kwa Sasa zimejifunga

"Tarura watuchongee Barabara  maeneo yetu mengi ya wilaya sasa hivi hayapitiki ,walichukue hili Kama dharura hasa katika kipindi hiki Cha Corona,ubovu wa miundombinu ya barabara ni tatizo ambalo limeanza miaka miwili hii awali  Barabara zote zilikuwa zinapitika kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwakuwa zilikuwa zinachongwa ,"amesema diwani wa MihutaHamis Mfaume.



Madiwani wakipuliziwa dawa kabla ya kikao Cha baraza



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2