MHADHIRI CHUO KIKUU ASEMA NI VIGUMU SANA KWA MAZINGIRA YA SASA KUZUNGUMZIA MTU ANAYEWEZA AKASIMAMA AKAWA BORA KULIKO RAIS MAGUFULI... | Tarimo Blog

MHADHARI wa Chuo Kikuu Saint John jijini Dodoma Dk.Alfred Sebahene amesema kwamba ni vigumu sana katika mazingira tuliyonayo kwa sasa kuzungumzia mtu anaweza kusimama akawa bora kuliko Rais Dk.John Magufuli.

Akizungumzia kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk.Magufuli ,Dk.Sebahene amefafanua kuwa ni vigumu kwa sababu wananchi wameona matokeo chanya ya jitihada za Serikali hii ya Awamu ya Tano na kusisitiza kuna jitihada kubwa sana na mambo yanayoonekana ndio ambayo Mtanzania anataka kuyazingatia zaidi.

"Mtanzania anataka kusikia huduma za afya zimeboreshwa, mtanzania anataka kuona maji yanapatikana, mtanzania anataka kuona yuko salama na anafanya kazi kwa uhuru na amani.Kumbukumbu zinazonesha ziwe zitokanazo na tafiti au kumbukumbu za mashirika ya kidunia ya habari ya maendeleo ya Tanzania na yale yaliyofanyika kwa miaka mitano.

"Mambo haya huwezi kuyabeza, kwa hiyo sidhani kama ni rahisi kumuonesha mtu kidole na kusema huyu anaweza akasimama na akafanya makubwa zaidi , vigumu kusema sitaki kuzungumzia zaidi masuala ya kisiasa, lakini rekodi na sisi wanazuoni tunaona mambo makubwa yanayofanyika na sauti kwenye jamii nadhani iko wazi , inasema kuna hatua kubwa tumepiga wakati huu,"amesisitiza.

Dk.Sebahene ameeleza kuwa lakini unapoona miradi mikubwa ikitimizwa maana yake unazungumzia udhibiti wa hali ya juu , udhibiti unaoridhisha wa yale mapato yanayopatikana katika nchi.Matumizi ambayo hakuna mianya ya upotevu.

"Habari ya kudhibiti suala zima la rushwa na mambo ya ufisadi, kuifanya Serikali iwe katika mfumo mzima wa utendaji, kuongezeka kwa nidhamu ya kazi katika serikali na vyombo vyake, mkazo katika kuhakikisha ya kwamba maadili yanazingatiwa, hivi ni vitu ambavyo vimewekewa mkazo kwa muda wa miaka minne,kuona ongezeko la nidhamu na huwezi kubeza ukilinganisha na hali ilivyokuwa katika kipindi kilichopita,"amesema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2