NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO
Mtoto mwenye umri wa miaka tisa na mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Likuyuseka wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma Jeska James Kifaru anaomba kutoka kwa wasamaria wema kumsaidia mchango wa fedha ili aweze kwenda matibabu ya moyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya wazazi wake kutokuwa na uwezo wa kumfikisha katika hospitali hiyo.
Akiongea akiwa katika ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Jeska alisema anaomba msaada kwa wasamaria waweze kumchangia fedha ili aweze kwenda kutibiwa moyo katika hospitali ya taifa muhimbili baada ya wazazi wake kushindwa kumpeleka huko kutokana na kipato duni.
Mama mzazi wa Jeska aitwaye Stamili Abdallah Gehu alisema walifika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuomba kibali cha mkuu wa wilaya cha kuomba kuchangisha mchango fedha na wakafanikiwa kupata kibali hicho na sasa wanapita mitaani kuchangisha fedha hizo ili waweze kumpeleka kijana wao hospitali.
Stamili alisema walimpeleka kijana wao matibabu katika kituo cha afya Namtumbo mwezi januari mwaka huu na kasha kushauriwa na daktari wampeleke hospitali ya peramiho na walipofika katika hospitali ya peramiho aligundulika na tatizo la moyo hivyo akapewa dawa za kutumia mwezi mzima na alipomaliza alirejea katika hospitali hiyo tarehe 28 mwezi huo januari na kushauriwa kumpeleka kijana wao huyo hospitali ya Taifa muhimbili.
Hata hivyo wanaendelea kutumia dawa kutoka katika hospitali ya peramiho huku wakimwona kijana wao huyo akibadili rangi na kuwa Mweusi badala ya rangi yake ile ya awali kuanza kutoweka kila kukicha .
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Likuyuseka Bonifasi Sichela alisema mwanafunzi wake Jeska anahudhuria shule na kuipenda shule licha ya kuwa mdhaifu na kutoonesha furaha mara kwa mara darasani kwa kusumbuliwa na moyo lakini anafanya vyema masomo yake.
Wazazi wa Jeska ,James Flavian kifaru naStamili Abdaallah Gehu wanaishi katika kijiji cha Likuyuseka ambao kipato chao ni duni wanawaomba wasamaria wema msaada wa fedha kupitia namba zao za simu ya mkononi 0715490997 simu waweze kumpeleka mtoto wao hospitali taifa muhimbili.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment