Mzeewa miaka 75 auawa na kufungwa kamba kuonesha alijinyonga | Tarimo Blog


Na Amiri kilagalila,Njombe
Mzee Arusha Nziku (75) mkazi wa wilaya ya Wanging’ombe mkaoni Njombe,amekutwa amefariki nyumbani kwake huku akiwa amefungwa kamba ndani ya nyumba yake kuonyesha emejinyonga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema waliotekeleza mauaji hayo walitumia kamba kumfunga na kuonyesha kama amejinyonga.
“Ni mzee ambaye amekufa akiwa nyumbani kwake na hawa wauaji walichokifanya ni kwamba baada ya kumuua wakamfanya kama amejinyonga,ile kamba wameifunga lakini kwa ufupi wa lile jingo na urefu wa ile kamba inaonyesha kifo ni cha mashaka”alisema Hamis Issa
Aidha amesema mpaka sasa jeshi la polisi limeingia kazini kuhakikisha ni kitu gani kilicho sababisha kifo cha mzee huyo.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2