Njombe:Waumini wa kanisa la KKKT watakiwa kuvaa barakoa wanapoingia kanisani | Tarimo Blog

Na Amiri kilagalila, Njombe
WAUMINI wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya kusini,wametakiwa kuhakikisha wanavaa barakoa wanapofika ibadani.

Wito huo umetolewa na askofu wa kanisa hilo dayosisi ya kusini Dkt,George Fihavango mara baada ya ibada ya Jumapili katika kanisa la hilo usharika wa Mji Mwema mjini Makambako,ambapo amesema kuwa waumini wote wanatakiwa kuvaa barakoa wanapokuwa ibadani ili waweze kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Aidha ametoa wito kwa wakuu wa majimbo na wachungaji wa kanisa dayosisi ya kusini kuhakikisha waumini wote wanavaa barakoa wanapokuwa ibadani.

Amesema licha ya tahadhari ambazo zimeendelea kuchukuliwa na waumini wa madhehebu mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) kwa kukaa umbali wa mita moja na nusu hadi mbili na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabun,lakini ni wajibu kila muumini kufuata taratibu mbali mbali za kujikinga na virusi hivyo.

Amesema waumini wote wanatakiwa kutambua kuwa kutokutii maelekezo yanayotolewa na serikali ni kutokumtii Mungu, hivyo ni lazima wachukue tahadhali zote zinazotolewa na wataalamu wa afya badala ya kumwomba Mungu pekee.

Naye askofu msaidizi wa dayosisi hiyo Dkt Gabriel Nduye na kaim mkuu wa jimbo la Makambako mchungaji Lyosi Mwalyosi wamesema utekelezaji wa agizo hilo la kila muumini kuvaa barakoa linaanza mara moja kuanzia sasa na wamewataka waumini wote kulipokea hilo kwa kulifanyia kazi kwa haraka.

Hata hivyo baadhi ya waumini wa kanisa hilo,akiwemo Robart Bimbiga ,Rehema Goharimu na Maria Gomano wamesema kuwa endapo washarika wote watavaa barakoa itasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na virusi vya Corona.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2