NUNUA KINYWAJI BAA,CHUKUA KANYWEE NYUMBANI...UKIKAIDI TUNAKUCHUKULIA HATUA- DC MJEMA | Tarimo Blog

 Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKATI idadi ya wagonjwa wa Covid-19 nchini ikifikia 147, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imetangaza kupiga marufuku mikusanyiko ya watu kwenye baa zote ndani ya wilaya hiyo na kwamba wanywaji watalazimika kununua vinywaji na kwenda kunywea majumbani.

Marufuku hiyo imetangazwa leo Aprili 17 mwaka huu wa 2020 ,hivyo wamiliki na wahudumu wote wa baa wanatakiwa kufuata maelekezo hayo ambayo ni moja ya mkakati wa Kupambana na virusi vya Corona.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari,  amesema uamuzi huo unalenga kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa waendesha baa hizo, kuuza  vinywaji hivyo lakini lakini mnunuzi lazima akanywee nyumbani."Atakayekaidi agizo hili atachukuliwa hatua".

Mjema amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuzingatia maelekezo hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mwendeshaji wa baa na mtu yeyote atakayeonekana kwenye eneo la baa akiendelea kunywa wakati agizo hilo limeshatolewa.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2