Taasisi ya Wipahs na Medewell yaipatia Mloganzila msaada wa vifaa vya usafi | Tarimo Blog


Pichani ni baadhi ya msaada uliotolewa hospitalini hapa.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa MNH-Mloganzila Sr. Redemptha Matindi (kushoto) akifanya majaribio namna ya kutumia kifaa cha kunawia mikono kilichokabidhiwa leo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wipahs na Medewell Bw. Jaabir Rajani.

Hospitali ya Taifa Muhimbili–Mloganzila imepokea msaada wa vifaa vya usafi pamoja na kunawa mikono kutoka kwa Taasisi ya Wipahs na Medewell ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona (Covid-19).

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wipahs na Medewell, Bw. Jaabir Rajani ametaja aina ya vifaa mbalimbali vilivyokadhiwa kuwa ni pamoja na ndoo kwa ajili ya kudekia, kifaa maalum cha kunawa mikono bila kushika, ndoo za kuweka taka (dustbins) na maji ya kunywa kwa ajili ya wagonjwa katoni 400.

“Tumeguswa kuleta msaada huu ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano yanayoendelea dhidi ya ugonjwa huu hatari, tunaimani kuwa njia sahihi na salama ya kujikinga afya zetu na watoa huduma ni kwa kunawa mikono kabla na baada ya kupata huduma” amesema Bw. Rajani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Redemptha Matindi amewashukuru wadau hao kwa kuguswa kutoa msaada na ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kujitoa kusaidia taasisi za afya katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

“Kwa niaba ya uongozi wa hospitali tunawashukuru kwa kuguswa kutoa msaada huu ambao umekuja wakati muafaka hivyo nawasihi taasisi zingine ziendelee kusaidia taasisi za afya ili kuimarisha utoaji huduma” amesema Sr. Matindi.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2