TAKUKURU Njombe yaokoa Bilioni 1,769,161,693.31 kwenye chunguzi zinazohusu AMCOS na SACCOS | Tarimo Blog


Na Amiri kilagalila,Njombe

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Njombe imefanikiwa kuokoa Bilioni 1,769,161,693.31 kutokana na chunguzi zinazohusu AMCOS na SACCOS mkoani humo.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Bi,Domina Mukama ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari-Machi 2020.

“Jumla ya SACCOS na AMCOS 85 katika mkoa wa Njombe zilikuwa zinachunguzwa 14 Makambako,6 Ludewa,19 Makete,13 Wanging’ombe,35 hapa Njombe mjini zikidaiwa jumla ya Tshs.7,965,449,650.04 ambapo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2020 tumefanikiwa kuokoa kiasi cha Tshs. 1,769,161,693.31”alisema Mukama

Mukama amesema hatua ni kutokana na agizo la Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa ili kufuatilia fedha za wananchi ambao ni wanachama wa vyama vya ushirika vya msingi AMCOS na SACCOS ambazo zimeliwa au kufanyiwa ubadhirifu na viongozi wa taasisi hizo.

Aidha amewapongeza wananchi wote waliojitokeza kulipa madeni hayo huku akiagiza waliosali na ambao bado hawajajitokeza wajitokeze wenyewe kwa hiari yao. 
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Bi,Domina Mukama

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2