Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema wanatarajia kupata zaidi ya tani Mia nane ya zao la ufuta kwa msimu huu 2020
Ameyasema hayo alipotembelea shamba la mkulima Hassan Chipyangu (udede) ambalo lipo katika kata ya Michenjele
"Msimu huu tunatarajia kupata zaidi zao la ufuta baada ya mwitikio wa wakulima kulima zao hilo hapo awali wakulima walielekeza nguvu zao kwenye zao mo ja lakini Sasa wanafunguka kwa kulima mazao mengine,"amesema Waryuba
Aidha amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya kilimo Cha ufuta kwani kimeonekana kustawi katika Wilaya hiyo badala ya kutegemea zao la korosho pekee
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka amesema walitenga kiasi Cha Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya mbegu ambazo walipewa wakulima kwa makubaliano kuwa wakivuna warudishe mbegu hizo ili wapewe na wengine
"Kwa Hali ambayo naiona katika mashamba mengi ya ufuta tuliyoyatembelea ndani ya Hamashauri,ufuta umeonekana kustawi hivyo ili uzalishaji uendelee kuwa wa viwango vikubwa tunatarajia kuanza kuwashindanisha maafisa ugani wa kata zote za Halmashauri,"amesema Msomoka
Hata hivyo amesema watawashawishi wananchi katika mfuko wa fedha za akina mama,vijana na walemavu kulima zao la ufuta badala ya kubuni miradi ambayo badae inawashinda kurejesha fedha hizo kwa wakati

Dc Waryuba (kulia)akiwa na Mkurugenzi Said Msomoka (kushoto) walipotembelea shamba ekari 10 la mkulima Udede
Shamba la mfano lililopo Kijiji Cha Michenjele Wilaya ya Tandahimba
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment