TMDA yakabidhi michoro ya jengo la ofisi yake ya Kanda ya Kati Dodoma kwa mkandarasi NHC | Tarimo Blog

  Pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Bw. Adam Fimbo akimkabidhi Injinia Haikamen Mlekio wa NHC michoro ya ujenzi wa ofici ya Mamlaka utakaofanyika katika eneo Ilazo jijini Dodoma. Ujenzi wa ofisi hiyo ambao unatarajiwa kuchukua miezi 12 toka tarehe 18 Aprili 2020  utakamilika tarehe 17 Aprili 2021.

Kukamilika kwa ujenzi huu kutaiwezesha TMDA kutekeleza majukumu yake kiufanisi katika kuhudumia mikoa ya Kanda ya kati ambayo inajumuisha Dodoma, singida na Morogoro.

TMDA ambayo hapo awali ilijulikana kama TFDA ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kusimamia ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

 Lengo la taasisi hii ni kulinda afya ya Jamii dhidi ya madhara yanayoweza kutokea baada ya matumizi ya bidhaa hizi

Hafla ya makabidhiano ya michoro katika kiwanja cha TMDA yalishuhudiwa na Mtaalam Mshauri toka Ardhi University Bi. Neema Mbwambo
Hafla ya makabidhiano ya michoro katika kiwanja cha TMDA yalishuhudiwa na Mtaalam Mshauri toka Ardhi University Bi. Neema Mbwambo
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2