Wadau wa maendeleo Njombe wafika vijijini kutoa elimu dhidi ya Covid-19 | Tarimo Blog

Na Amiri kilagalila, Njombe
KUTOKANA  na elimu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya Corona (COVID-19) kutowafikia vyema wananchi waishio maeneo ya vijijini wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Njombe wameanza zoezi la kwenda kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Miongoni mwa wadau hao ni Johson Mgimba na Lawi Mnyanga ambao wamefika katika kata ya Madilu wilayani Ludewa mkoani Njombe na kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali kupitia maeneo ya ibada ambapo wamewataka wananchi kufuatilia vyombo mbalimbali ili kufuatilia taarifa za wataalam wa afya ili kujikinga na virusi vya Corona

Kwa upande wake Mwenyekiti wa utume na uinjilisiti taifa kanisa la Anglican Tanzania, Nicolaus Mgaya amewataka waumini wa kanisa hilo kufuata sheria za wataalam wa afya ikiwemo kuvaa barakoa wawapo kwenye maeneo ya ibada pamoja na kukaa umbali wa mita moja ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Baadhi ya wananchi waliofikiwa na elimu hiyo wamewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo vijana kutoka kata ya Madilu huku wakiwa tayari kukabiliana na ugonjwa huo kwa kufuata kanuni za afya.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2