Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
WANAWAKE watatu akiwemo mama mlezi wa binti mwenye umri wa miaka 12, Scholastica Charles (34) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kumfanyia ukatili binti yake (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali.
Mbali na Scholastica, washtakiwa wengine ni Salma Hamisi (25) na Happy Joshua (44), ambapo wote ni wafanyabiashara wanaoishi Kitunda jijini Dar es Salaam.
Akisoma hati ya mashtaka leo, Wakili wa Serikali Faraji Nguka amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu kuwa, Februari 24 mwaka 2020 huko Kitunda Machimbo wilayani Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa hao wakiwa walezi wa binti huyo walimshambulia na kumsababishia maumivu makali.
Hata hivyo, washtakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo na ni mshtakiwa Happy tu ndio amefanikiwa kupata dhamana huku wengine wameshindwa kutimiza masharti na wamerudishwa rumande. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 30, mwaka 2020.
Watuhumiwa wakifishwa Mahakamani Kisutu leo,jijini Dar

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment