RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kufuatia kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Agostine Mahiga.
Balozi Mahiga alifariki nyumbani wake Mjini Dodoma baada ya kuugua hafla ambapo alipofikishwa hospitali tayari alikwishapoteza uhai na kuzikwa jana Mkoani Iringa.
Katika salamu hizo Dk. Shein alisema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Agustine Mahiga kilichotokea Mjini Dodoma.
“Kwa niaba ya watu wa Zanzibar na Serikali natoa mkono wa pole na rambirambi kwako Mheshimiwa Rais, familia ya marehemu pamoja na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msiba wa kuondokewa na kiongozi aliyekuwa na upendo wa nchi yetu”, ilieleza sehemu ya salamu hizo za rambirambi alizozituba Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alisema Balozi Mahiga ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi katika shughuli za kimataifa ikiwemo Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na taasisi nyengine.
Dk. Shein alisema kuwa Balozi Mahiga alikuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo na kudumisha umoja, amani na upendo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata misingi ya Katiba na Sheria.
Rais Dk. Shein alimuomba Mwenyezi Mungu awajaalie wafiwa na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania moyo wa subira katika kipindi hichi cha msiba.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment