Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Mtafiti wa Dawa za asili aliyejulikana kwa jina la Rose Roberty (changa Muja) ameiomba Serikali kumsaidia kupima dawa aliyogundua na kuifanyia majaribio kuona kama inatibu ugonjwa wa Corona (Covid-19)
Akiongea na waandishi wa habari leo nyumbani kwake,Rose alieleza kuwa ameweza kugundua dawa ambayo inaweza ikatibu ugonjwa huu ambao unaotikisa dunia ,na anaimani kabisa dawa hiyo itaweza kuponya ugonjwa huo.
Alisema dawa hiyo inatokana na mchanganyiko wa miti shamba mbalimbali iliopo hapa nchini,ambayo ameichanganya pamoja na viungo mbalimbali vikiwemo limao ,tangawizi kitunguu swaumu na vinginevyo .
Alibainisha kuwa virusi vya ugonjwa huu wa Corona vinashambulia Sana Kinga za mwili na iwapo mtu atajitaidi kutumia vitu vya kuboresha na kuongeza Kinga hizi itasaidia kutopata ugonjwa huu.
" Dawa hii Kama nilivyowaambia ni mchanganyiko wa vitu vingi ambavyo ni miti shamba ,na nimechanganya miti ya Aina mbalimbali ,unajua zamani kule kwetu Singida kunamti ambao tulikuwa tukiumwa Sana kifua Cha kubana au mafua tunatumia na mti huu pia unapendwa na wanyama Sana hivyo nimeuchukuwa na nikachangaya na mingine ndio nikaitengeneza hii dawa"alibainisha Rose
Alisema kuwa tayari yeye na familia yake wameshaitumia dawa hii ambapo alisema kuwa awali ,kunamtu mmoja wa familia yake alikuja nyumbani akiwa na dalili zote za ugonjwa wa Corona na ndipo alipokumbuka miti hiyo alichukuwa akaichanganya na alivyompa alipona ,huku akibainisha mbali na hao pia alishawapa baadhi ya watu ambao walikuwa wanabanwa Sana vifua na wanaendelea vyema.
Alisema awali alipeleka dawa hii Katika sehemu husika ikiwemo mamlaka ya chakula na dawa lakini akusaidika kwani Hawakumsikiliza Bali walimpuuzia na ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kuamua kuwaita waandishi ili imsaidie kuomba serikali ,iichukue dawa hii na kuifanyia utafiti.
Aidha alimshukuru Rais Wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli kwa kuweza kuwaruhusu Waganga wa tiba za asili nao kushiriki Katika Zoezi zima la kuangalia namna ya kupata dawa za ugonjwa huu wa Corona pamoja na namna anavyokuwa na Imani ya dawa za miti shamba pamoja na kumuamini Mungu.
Aliongea kuwa anaimani kabisa dawa anayoitengeneza inaweza ikatibu na kukinga watu kutokupata ugonjwa huu na iwapo serikali itaipima na kuikubali Basi atapenda itambulike kwa jina la MJOUNJOU.
Alitoa wito kwa wananchi pamoja dawa zinaendelea kugunduliwa ni vyema waendelea pia kufuata tahathari zinazotolewa na wataalam wa afya.
Picha ikionesha Mtafiti wa dawa za asili aliyejulikana kwa jina la Rose Roberty (changa Muja) akionesha dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona 19 aliyogundua ambayo ameiomba Serikali imsaidie kuichukuwa na kuipima na kufanyia majaribio (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment