PROF. KABUDI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI | Tarimo Blog

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi katika picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali WilbertA. Ibuge
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimuelezea jambo Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge
Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge
**********************************
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusu mahusiano baina ya Tanzania na Italia.

Aidha, walitumia mazungumzo hayo kujadili hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya Italia katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19.

Mhe. Waziri alifahamisha kuwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kwenye mapambano ya ugonjwa huo zimezingatia mazingiria na hali halisi ya Tanzania pamoja na nchi jirani zinazozunguka Tanzania.

Kwa upande wake Balozi Mengoni alipongeza juhudi hizo za Serikali ambapo alifahamisha kuwa Serikali yake ya Italia inaziunga mkono na kwamba ipo tayari kutoa ushirikiano pale itakapohitajika kufanya hivyo.

Viongozi hao walikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya Mataifa hayo mawili ambao umejikita katika sekta za elimu, afya, utalii pamoja na biashara na uwekezaji

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2