Rais Magufuli Awaasa Watanzania kutunza chakula | Tarimo Blog

Rais John Magufuli amewaasa watanzania kutunza chakula kwani kutakuwa na uhitaji mkubwa kwa nchi za Afrika na mataifa mengine yalijifungia bila kulima sababu ya virus vinavyosababisha Corona.

Akihutubia wananchi leo Dodoma katika uzinduzi wa majengo ya ofisi za ikulu Chamwino, Rais Magufuli amesema watanzania wasikubali kulanguliwa mazao yao waliyozalisha kwa wingi mwaka huu.

" Nawaasa watanzania mtunze chakula na muuze kwa bei ya juu mazao mliyostawisha kwa wingi mwaka huu. Nawaambia watwange kwa bei wanunuzi. Nasema watwange," amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kuanzia sasa hadi miaka miwili ijayo kutakuwa na uhaba wa chakula ktk nchi nyingi hivyo ni fursa kwa watanzania kuuzia nchi hizo chakula.Tanzania kwa mwaka huu imezalisha chakula kingi mno na nchi ina akiba ya kutosha kwa hiyo wakulima wataweza kuwauzia majirani chakula.

Nchi nyingi Afrika zilitumia ugonjwa unaosababishwa na virusi kufungia wananchi wao ndani badala ya kuwafungulia kulima hivyo watapata taabu sana kwa njaa.

Tayari wananchi wa mataifa mengine wameanza kuugua vipindipindu sababu ya kufungiwa ndani na kukosa chakula.Tumeskia juma lililopita wananchi wa Kenya 13 walivyougua kipindupindu sababu ya kufungiwa bila huduma nzuri za vyoo.

Tumeona katika vyombo vya habari Raisi wa Uganda Yoweli Museveni akiwafundisha waganda kubadili ulaji na kula tonge dogo la ugali ili kuishi.

Tumeskia nyingi na majirani zetu wanavyoangaika kupata mlo wa kushiba.

Tanzania kama nchi ya ukombozi itaziuzia nchi hizo chakula ili wananchi wake wasife na kuugua utapiamlo maana tunategemeana sana katika nyanja mbalimbali

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2