TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YATUMA SALAMU ZA POLE KWA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MAHIGA | Tarimo Blog


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb) kilichotokea leo alfajiri Mei 01, 2020 Jijini Dodoma.

Tume inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuondokewa na kiongozi  mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika nyanja za Kimataifa kwa miaka mingi.

Aidha,  Tume inatoa salamu za pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Wabunge, Wafanyakazi wa Wizara  ya Katiba na Sheria, familia ya Marehemu na wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Tume ikiwa taasisi iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria inaungana na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu na inawaomba wanafamilia wote kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi, Amina.


Imetolewa na:


Jaji (Mst) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Mei 01, 2020

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2