Huduma za simu zinavyoisaidia Tanzania kukuza uchumi wake | Tarimo Blog

Mashaka Meela, Dar es Salaam
TAKWIMU za uchumi za hivi karibuni zinaonesha kuwa kuna kila sababu ya kuwa na matumaini na hali ya uchumi wa nchi yetu. Kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), uchumi wa Tanzania unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.2 kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Takwimu hizi zinaakisi utafiti wa awali uliofanywa na Taasisi ya Legatum ya nchini Uingereza ambao ulieleza kuwa uchumi wa Tanzania ni moja kati chumi zinazokua kwa kasi zaidi Afrika Mashariki.

Utafiti huo ulibainisha baadhi ya sababu zinazouwezesha uchumi kukua kwa kiwango hicho kuwa ni pamoja na mchango wa serikali katika uwekezaji kwenye sekta mtambuka na kujenga mazingira ya uchumi kuelekea katika mapinduzi ya viwanda.

Taarifa za uchumi za hivi karibuni zimeripoti juu ya vichocheo hivyo ambavyo ni pamoja na ujenzi wa barabara, kukarabati na kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ambayo inawezesha uingizwaji na usafirishwaji wa bidhaa nje ya nchi kwa urahisi.

Utafiti wa taasisi hiyo pia umeonesha kuwa ukuaji wa uchumi umechangiwa pia na maboresho ya watu kuunganishwa kupitia simu za mkononi, intaneti na akaunti za benki. Upatikanaji wa huduma hizi umekuwa jambo la msingi katika kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia uchumi wa Tanzania kuwa mtambuka katika ukanda huu.

Maendeleo ya kuwaunganisha wananchi yamewezeshwa na jitihada mbalimbali za serikali pamoja na sekta binafsi.

Kwa miaka ya hivi karibuni, mchango wa sekta binafsi umekuwa ukiongozwa na uwekezaji mkubwa wenye tija wa kampuni za mawasiliano ya simu. Kwa mfano, takwimu zinaonesha kuwa sekta hiyo imewekeza zaidi ya TZS 6 trilioni nchini katika maeneo yahusuyo maboresho ya matandao pamoja na kuleta 4G.

Uwekezaji huo umekuwa na mafanikio makubwa sana kwa jamii, mfano, Tigo Tanzania, mmoja wa watoa huduma wakubwa zaidi Tanzania, imesaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha mfumo wa fedha jumuishi kupitia huduma yake ya fedha, Tigo Pesa. Huduma hii ambayo ni rahisi na ya haraka kutumia imesaidia idadi kubwa ya watu ambao hawakuwa wakitumia huduma za kibenki kwa kuwapatia njia ya kuaminika ya kupata huduma za kifedha. 

Aidha, Tigo imekuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara kwa kuwawezesha kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa kupitia huduma ya Tigo Business. Huduma hiyo imewezesha kampuni kubwa na ndogo kuunganishwa na kutumia intaneti, jukwaa la kuhifadhi taarifa pamoja na huduma za simu zinazoendana na mahitaji yao.

Huduma za Tigo ni moja ya mifano mingi ambayo sekta ya mawasiliano ya simu inafanya kazi kuchochea ubunifu na kukuza kiwango cha wananchi kufikiwa na huduma hivyo kukuza uchumi wa nchi.

Ni wakati sahihi sasa kulinda maslahi ya sekta hiyo katika miaka ijayo. Kuchochea uwekezaji zaidi na kulinda mazingira ya usimamizi wa soko ni njia kuu mbili zitakazotuhakikishia kuwa sekta hiyo inaendelea kukua na kunufaisha nchi yetu.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2