WAZIRI AMJULIA HALI KIJANA DEOGRATIUS MIANGA | Tarimo Blog

Mheshimiwa Majaliwa akizungumza na  Mianga  hospitalini hapo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa  MOI Dkt. Respicious Boniface, (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Ijumaa Julai 24, 2020) alimjulia hali kijana Deogratias Mianga mkazi wa Singida ambaye amelazwa katika Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya matibabu.

Waziri Mkuu alimuona Deogratias kupitia vyombo vya habari akiomba msaada wa matibabu kutokana na matatizo ya mgongo.  Waziri Mkuu aliguswa na hali ya Deogratius na tarehe 02/07/2020 alimuwezesha kufika MOI na kufanyiwa upasuaji tarehe 06/07/2020. 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2