Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mbeya
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bara Philip Mangula amesema kuwa Rais Dk.John Magufuli ambaye kwa sasa anaomba tena dhamana ya kuongoza nchi ndio mbeba maono ya muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Nyerere.
Mangula amesema hayo mbele ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Magufuli ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua yote ambayo yanatendeka sasa ni kwasababu nchi ina amani na hata mikusanyiko yote ipo kwasabaabu nchi ina amani bila amani hakuna kinachoweza kufanyika.
"Rais wetu ni mbeba maono ya Mwalimu Nyerere, baada ua uhuru tupambane na umasikini, ujinga na maradhi pamoja na dhuluma, Rais wetu umebeba kijiti cha kusukuma hayo kwa spidi, wabunge wameleza kwenye majimbo yao ambayo yamefanyika na wameridhika umefanya makubwa.
Wakati huo huo amesema kuwa wapinzani ambao wamekuwa wakipinga kila kitu ambacho kimefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, basi wangepinga na watoto wao kwenda shule ambako inatolewa bila malipo lakini wanafaidika na yale yote ambayo Rais amefanya.
Pia amesema kwamba kuwa njia nzima tangu Igawa watu walikuwa wengi wakimsalimia Dk.Magufuli. "Nilijua hakutakuwa na watu, nilidhani alishawasilimia. Nadhani wingi wao pia ni kukiri makosa waliyofanya mwaka 2015, niwaombe sana jinsi ambavyo tumejazana hapa tukajaze na kwenye sanduku la kura.
"Wenzetu wameingia hofu, wanasema watalinda kura, sheria inakataza, ukipiga kura nenda nyumbani, mawakala wapo kwa ajili ya kulinda kura zote, kila chama kina wakala , hawa wanaosema watalinda kura maana yake wanataka kufanya vituko vyao.Sisi wana CCM tukapige kura na kisha waendelee kutulia nyumbani. Siku ya kupiga kura ni Jumatano na hivyo tulidhani watu wanachelewa nyumba za ibada, mapumziko yako nenda kituoni kupiga kura,"amesema Mangula.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Jacob Mwakasole amesema kufika kwa Dk.Magufuli katika mkoa huo wananchi wamejawa na furaha."Naomba niseme watu wa Mbeya walikuwa wanaomba kila siku baada ya kusikia kuna ujio wa mgombea urais wa CCM atakuja Mbeya tukawa tunasubiri kwa hamu.Nakumbuka siku moja wakati nawasilisha majina ya waliokudhamini, wananchi walisema hauna sababu ya kuja Mbeya kwasababu umeshapita ila wanahamu ya kukuona.
"Hakuna zawadi nyingine ya kukupatia zaidi ya kura za heshima Mkoa wa mbeya, Mbeya imebadilika na sasa ni ya kijani nakuonesha kwamba tunakupenda hatuwezi kufanyia kwenye viwanja , tumeamua kukuleta hapa Uwanja wa Ndege wa zamani, hiyo ndio shukrani ya watu wa Mbeya, tunakutakia heri ba baraka tele, Magufuli unawapenda wanyonge, mtu mwadilifu na mwaminifu kila unachokusanya unapeleka kwenye maendeleo,"amesema Mwakasole.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bara Philip Mangula
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment